Kamati ilipata nafasi ya kuonana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kingwangalla. Amefurahi kujua na kuona kuna umoja wetu wenye malengo ya uwindaji endelevu. Ataitisha kikao na watendaji wake likiwa na lengo la kujadili hoja msingi kama vile quota , sheria na kanuni za kutushirikisha n.k. Yeye mwenyewe atakuwa mwenyekiti wa kikao hicho. Alivutiwa sana na utaratibu wa Tacha na akaongeza kuwa Tacha imekuja wakati muafaka.

Aidha tunawashukuru wote waliotuwezesha kwa hali na mali kufika na kukaa Arusha. Tuendeleze moyo huo huo kwani kujenga chama chenye nguvu kunahitaji ushirikiano wa aina hii.