
Tulikuja Mtepera na kujadiliana na uongozi wa Kijiji na walieleza shida ya kubwa ya maji, ambayo walikuwa wakitegemea maji kutoka mto wa MATANDU ambao hujaa kwa msimu. Kina mama na Watoto walikuwa wakienda mwendo mrefu kufuata maji. Sisi kama wanachama wa TACHA tulichukua tatizo na kuliwakilisha kwa wanachama wenzetu, ambao waliafiki kwa pamoja kuchangia. Katika muktadha huu, sina budi kukiri mchango mkubwa uliotolewa na bwana Naif Abri, mkurugenzi wa ASAS (Mwanachama wa TACHA) pamoja na mchango ya hali na mali kwa wanachama wengine wa TACHA uliowezesha kupatikana kiasi cha Tshs 46,000,000/= ambayo yalikuwa makadirio ya kitaalamu ya kuwezesha kuchimba kisima. Kazi ya kuchimba kisima ilianza rasmi tarehe 21 Sept 2023 na ilichukua takribani siku tatu kuchimba na kupata maji takribani mita 200 chini ya ardhi, ujenzi wa miundo mbinu na uwekaji wa mfumo wa nguvu za jua na matanki ya kuhifadhia maji ulichukua takribani wiki tatu. Kazi hiyo ilikamilika rasmi 25 October 2023, na ilikuwa chini ya majiribio kwa kipindi cha mwaka mmoja. TACHA tulitoa pikipiki moja kwa ajili ya uhuduma za uhifadhi na pia ujenzi wa kambi ya muda kando ya mto Matandu, tukiwa na nia ya kutoa ajira kwa vijana kwa huduma wanayotoa kwa wawindaji wote.